Image
Image

Jinamizi lililokuwa limewatafuna Tunda man na Matonya Kwa kipindi cha Miaka nane Lamalizwa Leo Tena.


Picha ya pamoja ikiwa inamuonyesha mwanamuziki Matonya(Kushoto)Tunda Man (Kulia)wakiwa wamekumbatiana kwa ishara ya furaha baada ya kutofautiana kwa kipindi kirefu(Picha kwa hisani Leo Tena Clouds)
Bifu la muda mrefu takribani miaka nane lililokuwa likiwakabili wasani wa bongo flava nchini Tanzania kati ya matonya na tundamani leo hii limefikia ukomo kupitia kipindi cha leo tena cha Clouds Fm.
Ukomo wa bifu hilo umemalizika wakati ambapo tunda mani alipokuja kutambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ACHANA NA MIMI kwenye kipindi cha leo tena,ambapo pamoja na mambo mengine ilionekana kuwa kwa kipindi na hata tetesi na mashabiki wanafununu juu ya ugomvi wa Tunda man na Matonya ambao umefanya wawili hao kuwa wakikwepana katika sehemu mbali mbali na jambo ambalo lilitengeneza uadui kati yao kwa kipindi hicho kirefu.
Wakati tunda mani akiwa ndani ya studio za Clouds na ujio wake huo Mtangazaji wa Leo tena Husna Abdul  alimuuza tunda mani juu ya tetesi na uvumi juu ya kuwa na bifu na matonya kwamba hilo lipoje ambapo tunda alisema kuhusu bifu hana uhakika sana lakini yeye yupo radhi kama alikosea au alikosewa wasameheane yaishe huku akisema tena leo ni ijumaa kwahiyo kama matonya anasikia Basi akaswali na asamehe ikiwa kuna bifu.
Kwayeye binafsi matonya alitumia muda kujitetea na kusema yeye hana bifu wala tofauti yeyote na msanii mwenzie matonya ila hiyo imekuja kufuatia wimbo wa Vaileth ambao ulitamba sana aliokuwa kamtungia matonya ila tu matonya hakuwa wazi kusema ngoma hiyo nani aliyekuwa amemtungia.
Bila kupepesa macho wala unafiki wa aina yeyote haswa akitaka kujenga nyumba moja ya wasanii hao kati ya matonya na Tunda mtangazaji wa Leo tena Husna alimuuliza tunda kwamba ukisemacho kuhusu tonya nichakweli na je pengine akitokea hapa ama tukimuita unaweza kuongea naye,Tunda alisema leo niijumaa nakama ananisikia Matonya aje hapa studio aliongea Tunda kwa kujiamini akiwa Live kwa leo tena.
Baada ya muda simuda wakiwa hawajamueleza Tunda mani walimwendea hewani Matonya nahivyo kwa uadilifu wake matonya aliitikia wito nakufika studioni hapo kwa muda muafaka ambapo waliwekwa meza moja ikiwa ninia ya kuwa suluhisha kutokana na wao kukaa takribani miaka 7 hivi bila kuonana licha yakuwa wamekuwa wakionana kwambaaali sanaaaa tofauti nawao jinsi walivyokuwa.
Matonya aliweza naye kuweza kuweka utetezi wake mbele ya kadamnasi ambapo alisema kuwa yeye hakutungiwa ngoma hivyo ya Vaileth na Tunda ila yeyemwenyewe alifanya mambo hayo,lakini katika muendelezo wa mazungumzo yake aliweza kumsifia Tunda na kusema tunda ni mdogo wake sanaa ten asana na anaamini anauwezo anasema”Tunda yapo mambo aliyoyafanya kwenye wimbo wa Vaileth ambao umekuwa na mvutano kwahiyo tumeshirikiana naye kufanikisha,angetakiwa auimbe ila Produce akasema sauti yatunda bado kidogo kuimba wimbo huo.”Alisema Tonya Boy.
Tonya anasema kuwa hatasiku moja hawezi kumdharau Tunda Man kwakuwa ni mdogo wake tena watatu”Fikiria tuikienda nyumbani tunda anachinjiwa kuku na anakula mimi sili kwakuwa ni mdogo wangu woote nyumbani wanamjua na yani nizauidi ya mdogo wangu kwahiyo siwezi kujengeana uhasama na Tunda”Alisema Tonya.
Tonya anasenma tunda sio mbaya hata kidogo kwakuwa ni mdogo wake ila alichokuwa anaamini kupitia mgogoro huo wa muda ilikuwa inaonyesha kama tunda labda alikuwa anatumiwa na watu Fulani ila yeye kama yeye hakuwa akiamini kweli tunda ndio Yule wakipindi kile wa kufa na kupona anasema”Kwakuwa tunda ni mdogo wangu nimemsamehe kwakuwa akiwa nimwanao kakuyea kiganjani huwezi ukakata kiganja ila tu utaenda kukisafisha na kuendelea na mambo mengine”Alisema Matonya
Hata hivyo wasanii hao wawili wameweza kusameheana kwa moyo mmoja nahivyo matonya akiwa Live radioni alisikika akisema kwanza tukitoka hapa tunaelekea studio na mdogo wangu Tunda,ambapo kupitia mazungumzo hayo na msamaha huo inaonyesha kuwa wanataka kufanya ngoma ya pamoja inayodhihirisha kumaliza kabisa tofauti baina yo.
Tunda mani na matonya walikumbatiana na kupigwa picha ya pamoja huku wakiwa na furaha na hivyo kuondoka pamoja kuelekea Studio waliposema wanakwenda.
Kwa hatua hiyo nasi Tambarare Halisi Tumependa upatanishi huu na kila mmoja kuitikia wito ambao utawafanya kama kioo chja jamii kufika mbali zauidi ki mziki na kuweza kuitambulisha na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia muziki,Hii si kwa wasanii hawa tu bali na wengine ambao pengine wana migogoro niwakati wa kufungua ukurasa Mpya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment