Image
Image

Kikosi cha ulinzi wa Rais obama kinawachunguza maafisa wake wawili


Kikosi cha ulinzi wa rais wa Marekani kinawachunguza maafisa wake wawili waandamizi kwa kuhusika na tukio la kugonga gari katika Ikulu ya Marekani.

Msemaji wa Kikosi hicho, ameviambia vyombo vya habari tukio la ajali hiyo lilitokea wakati wa jioni tarehe 4 mwezi huu.

Gazeti la The Washington Post liliripoti kuwa maafisa hao waliendesha gari za msafara wa usalama baada ya kukesha wakinywa pombe kwenye sherehe.

Tukio hilo la ajali Ikulu ya Marekani, linaendeleza mlolongo wa matukio ya aibu yaliyohusisha kikosi hicho chenye jukumu la kumlinda Rais Barack Obama.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment