Image
Image

Mashirika ya Misaada yasema watoto 80 waliookolewa kwenye kambi ya Boko Haram hawana kumbukumbu ya majina na Walikotoka

Mashirika ya misaada yanasema watoto wapatao 80 waliookolewa kutoka kwenye
kambi ya kikundi cha Boko Haram huko Cameroon hawawezi kukumbuka hata majina
na walikotoka.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa misaada watoto hao wenye umri wa kati ya miaka
mitano na 18 walipatikana mwezi Novemba mwaka jana baada ya kampeni ya
wapiganaji wa kikundi hicho kuvuka mipaka na kuingia nchi jirani.
Kikundi cha Boko Haram kinapigana kutaka maeneo ya kaskazini mwa Nigeria
yawe taifa la kiislamu.
Hivi sasa kinadhibiti miji na vijiji kadhaa kaskazini mwa Nigeria na hivi
karibuni kikundi hicho kimeahidi utiifu kwa kikundi cha Islamic State
ambacho kimekamata maeneo makubwa ya Syria na Iraq.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment