Image
Image

Maziko ya Mbunge wa MBINGA Magharibi kufanyika leo Kijijini kwake LITUHI Ruvuma

Maziko ya Mbunge wa Jimbo la MBINGA MAGHARIBI Kapteni JOHN KOMBA yanatarajia kufanyika LEO Kijijini kwake LITUHI Wilayani NYASA Mkoani RUVUMA.
Maziko hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa huku wengi wakimwelezea Kapteni JOHN KOMBA kuwa kiongozi atakayekumbukwa kwa mchango wake katika kujenga uzalendo.
Baada ya kuwasili kwa mwili wa Marehemu KOMBA katika Uwanja wa Ndege wa RUHUWIKO ukitokea jijini DSM alipoagwa na Rais , Wabunge na wananchi katika viwanja vya Karimjee, msafara wa mwili wa Kapteni JOHN KOMBA ukaelekea katika Uwanja wa MAJIMAJI ambapo mamia ya wananchi walifurika kuuaga mwili wa mpendwa wao.
Wananchi na viongozi wa RUVUMA wanasema hawatasahau mchango wa marehemi Kapteni KOMBA katika maendeleo ya Mkoa wa RUVUMA.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amesema shughuli ya mazishi yatakayofanyika Kijijini LITUHI zitaanza Saa TANO Asubuhi pia itahudhuriwa na Rais JAKAYA KIKWETE, viongozi wengine wa Vyama vya Siasa na Serikali.
Hapo jana marehemu KOMBA aliagwa katika Viwanja vya KARIMJEE Jijini DSM na maelfu ya watu wakiwemo wasanii na wabunge.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment