Miili ya Watu waliofariki dunia
jana kutokana na ajali ya Basi la abiria la Majijna Express lililokuwa na Namba
za usajili T438 CDE lililokuwa limegongana na Lori la Mizigo lililokuwa
limebeba Kontena ambalo liliangukia basi hilo na kuua watu 42 katika eneo la
changarawe barabara kuu ya Iringa na
mbeya hatimaye idadi imeongezeka na
Kufikia Maiti 43 hadi sasa na majeruhi 26.
Kwa mujibu wa muandishi wetu
anasema kuwa kinachoendelea muda huu ni zoezi la kuwatambua maiti waliofariki
katika ajali hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya rufaa
ya mkoa wa iringa na hospitali ya wilaya ya mufindi ambapo ndugu wa marehemu
wameendelea kufurika hospitalini hapo kwalengo la kuwatambua ndugu na jamaa zao.
Hata hivyo Taarifa iliyotolewa
muda huu na mganga mkuu wa mkoa wa
iringa Dokta Robert Salim inaeleza kuwa
jumla ya maiti 26 wa ajali hiyo wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
iringa na maiti wengine 17 wamehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya
wilaya ya mufindi Mkoani Iringa
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa
idadi ya kufikia maiti hao 43 hadi sasa ni kufuatia mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo
aliyejulikana kwa jina la Oswald Mwinuka kufariki Dunia wakati akiendelea
kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa na majeruhi
wengine wawili wanangoja utaratibu wa rufaa ili kuwahamishia katika hospitali
ya taifa ya rufaa ya muhimbili huku wengine wakiendelea na matibabu kwenye
hospitali ya wilaya ya mufindi na hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa.
0 comments:
Post a Comment