Image
Image

Mjane wa baba wa taifa Mama MARIA NYERERE akanusha uvumi kuwa amefariki

Mjane wa Baba wa Taifa Mama MARIA NYERERE akukanusha Uvumi uliokuwa umeenea ndani na nje ya nchi kuwa Amefariki dunia jana kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Mwandishi  wa kituo cha Runinga cha TBC Nyumbani kwake Msasani Jijini DSM kufuatia uvumi huo, Mama MARIA NYERERE amesema alipokea simu kutoka kwa Mmoja wa watoto wake aliyeko Butiama na kutaka kufahamu kuhusu hali yake ya Afya baada ya kupata taarifa kupitia kwenye Mitandao ya Kijamii na simu ya Mkononi kuwa Mama MARIA NYERERE Amefariki Dunia.
Aidha Mbali ya kukanusha uvumi huo, pia Mama MARIA NYERERE amezungumzia kuhusu mauaji ya watu wenye ualbino yanayoendelea katika sehemu mbalimbali ya nchi na kusema kuwa Watanzania hawana budi Kumlilia mwenyezi Mungu ili aliepushe taifa na Balaa la Mauaji hayo yanayoendelea kutokea nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment