Image
Image

Mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam yasababisha adha ya usafiri na taharuki kwa waishio mabondeni.


Mvua zilizonyesha Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo  zimesababisha adha kwa wakazi mbali mbali ya jiji na hivyo kufanya hali ya usafiri kuwa mgumu na watu kuchelewa katika kulijenga taifa kwa wakati.

Pande za jiji kila mmoja amekuwa shuhuda wakusimulia hili ingawa hofu ya mvua hii inaonesha kuwaweka shakani wakazi wa mabondeni ambao serikali imekuwa ikiwasisitiza kuhama maeneo hayo kwakuwa sio rafiki mzuri wa maisha ya mwanadamu.

Baadhi ya nyumba maeneo ya msasani imeelezwa kuwa hali haikuwa shwari kwa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo ambayo maji yameweza kuingia majumbani mwa wakazi wa maeneo hayo nasehemu nyingine nahivyo kuharinu baadhi ya vitu,hali ambayo si nzuri sana na inatia hofu endapo mvua hiyo itaendelea.

Baadhi ya wakazi wa jiji wamezungumza na TAMBARARE HALISI Nakusema kuwa mvua hii inaonesha inanyesha kwa kusuasua kwani wakati inaonyesha kunyesha na hainyeshi hivyo ikinyesha bila kuwa na taarifa na kiwango cha mvua kinaweza kuleta madhara ya mafuriko kama yaliyokuwa yametokea na kuhatarisha maisha ya wakazi waishio mabondeni.

Hata hivyo wameiomba mamlaka ya hali ya hewa nchini kuweza kuzungumza nmamna mvua hizi zitakavyokuwa zikinyesha na hata ukomo wake ili kuweza kuchukua tahadhari mapema kabla hayajatokea makubwa.

Hata hivyo wameiomba mamlaka ya hali ya hewa nchini kuweza kuzungumza nmamna mvua hizi zitakavyokuwa zikinyesha na hata ukomo wake ili kuweza kuchukua tahadhari mapema kabla hayajatokea makubwa.
 Hivi ndivyo hali ionekanavyo kwa mvua iliyonyesha usiku wa muamkia leo hii katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam,Hapa Ni Bamaga Mwenge.
Na Chini hapo ni Baadhi ya Ghari zikiwa kwenye foleni leo asubuhi huku mvua ikinyesha Eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment