Image
Image

Naibu waziti TIZEBA amezihakikishia kaya zaidi ya 500 zenye makazi katika eneo la Mlima KISEKE jijini MWANZA kuwa makazi hayo ni salama kwa afya zao

Naibu Waziri wa uchukuzi DKT.CHARLES TIZEBA amezihakikishia kaya zaidi ya 500 zenye makazi katika eneo la Mlima KISEKE jijini MWANZA kuwa makazi hayo ni salama kwa afya zao kinyume na hofu iliyokuwa imetanda siku za nyuma kutokana na ujenzi wa rada katika mlima huo.
DKT.TIZEBA ametoa ufafanuzi huo mjini MWANZA kufuatia kaya hizo kujawa na wasiwasi zikitakiwa kuhama ili kunusuru afya zao.
Eneo la Mlima kiseke uliopo wilaya ya ilemela mkoani mwanza ndiko ambako rada ya kisasa ya utabiri wa hali ya hewa imejengwa ili kuimarisha shughuli za utabiri wa hali hewa katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Kujengwa kwa rada hiyo kumesababisha zaidi ya kaya mia tano zinazozunguka mlima huo kuendelea kuishi kwa hofu ya kukumbwa na athari zitokanazo na mionzi ya rada ikiwemo ugonjwa wa saratani.
Hofu ya wakazi hao imefuatia matamko kadhaa yaliyotolewa mwaka mmoja uliopita na viongozi wa serikali wakiwemo wa mamlaka ya hali ya hewa ya kuzitaka kaya hizo kuhama ili kunusuru afya zao.
Mwaka mmoja baada ya kauli hizo,naibu waziri wa uchukuzi DKT.CHARLES TIZEBA amekutana na waandishi wa habari jijini mwanza na kuwaondoa hofu wakazi hao kwa kueleza kwamba mionzi ya rada hiyo haina madhara kwa afya za wakazi wa eneo hilo swala lililo ungwa mkono na mhandisi LENY MGANGA ambaye ni meneja mradi wa rada hiyo.
Rada hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi billion 3 na milioni mia sita pia inakabiliwa na tishio la uendelevu kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kwenye mlima huo
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment