Image
Image

News:Moto uliozuka gafla wateketeza mabweni Chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Baadhi ya Mabweni ya wasichana  katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Campus ya Mabibo yameteketea kwa mot oleo hii ambapo chanzo chake  kinatazamiwa  kuwa ni hitilafu ya umememe.

Hata hivyo wanafunzi hao wameonekana wakililaumu jeshi la zimamoto kwa kuchelewa kuja kuzima moto hali iliyowachuukua muda wanafunzi hao kuzima moto huo wao wenyewe na hivyo gari la zimamoto lilivyofika kukuta tayari moto huo umeshapunguza makali yake.


Kwa mujibu wa waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho cha UDSM Bwana Gibson George amesema kuwa chanzo hakijajulikana mara moja juu ya kutokea kwa moto huo licha ya moto huo kusambaa maeneo mbalimbali ya hosteli hizo.

" Watu wa zimamoto tumewapigia simu  mapema sana ila wamechelewa kufika hadi muda huu ndio wamefika,tumejaribu kuuzima moto na umepungua kidogo japo bado unaendelea kwa baadhi ya vyumba" alisema Waziri Mkuu huyo.


 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment