Hii ndio picha ikiwaonyesha Abiria wa Majinja wakiwa wamekandamizwa na Kontena hilo eneo la Mafinga Mkoani Iringa ilipo tokea ajali hii leo(Tunaomba radhi kwa Muonekano wa Picha usiokuwa wakuridhisha)
Kwa mujibu wa
mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lilokuwa
linakwepa mashimo ya barabra na kugongana na basi hilo la abiria uso kwa
uso ambapo kamanda ya polisi mkoa wa iringa RAMADHA MUNGI amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na amesema atatoa taarifa kamili
baadae
Licha ya kamanda kukiri kupata taarifa juu ya ajali hiyo taayari baadhi ya mitandao mbali mbali imekuwa ikiripoti kuwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni kati ya 40 hadi 50,kwa habari kamili tutawafahamisha itakapo toka taarifa rasmi juu ya waliojeruhiwa na kupoteza maisha kadri tunavyo endelea kufuatilia.
0 comments:
Post a Comment