Image
Image

Rais Kenyatta wa kenya ameteketeza tani 15 za meno ya tembo kwa kutumia mafuta ya Petrol


Rais UHURU KENYATTA wa Kenya amewasha moto kuteketeza tani 15 za meno ya tembo baada ya lundo kubwa la meno hayo kumwagiwa mafuta ya petroli.

Meno hayo yamechomwa moto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani na miaka 25 tangu biashara ya meno ya tembo ipigwe marufuku kulinda wanyamapori waliokuwa katika hatari ya kutoweka duniani.

Bwana KENYATYTA amesema tangu wakati huo mapya yamekuwa yakiibuka kwenye masoko ya magendo ya nyala za wanyamapori na hivyo kutishia tembo na vifaru barani Afrika.

Kulingana na shirika moja la kimataifa la kuhifadhi wanyamapori lenye makao makuu yake London lilisema mwaka jana kuwa tembo 100,000 wameuawa barani Afrika kati ya mwaka 2010 na 2012 kutokana na ujangili.

Kwa sababu hiyo  Mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince WILLIAM ametaka uwindaji haramu upigwe vita na kukomeshwa ili kunusuru wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka barani Afrika na kwingineko duniani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment