Image
Image

NEWS ALERT: Rais kikwete afanya uteuzi wa wabunge


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10. 
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba, Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba. 
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
-         Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
-         Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
-         Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
-         Mhe. Janet Zebedayo Mbene
-         Mhe. Saada Salum Mkuya
-         Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
-         Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
-         Mhe. James Fransis Mbatia 
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
……………………………MWISHO……………………………….
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment