Image
Image

Rais KIKWETE avitaka vyombo vya habari kuzingatia maadili ya taaluma yao


Rais JAKAYA KIKWETE amevitaka vyombo vya habari kuzingatia maadili,kanuni na taratibu za uandishi wa habari .
Rais kikwete amatoa rai hiyo wakati wa uzinduzi wa studio mpya ya kurushia matangazo ya televisheni inayomilikiwa na kampuni binafsi ya SSTL inayojulikana kwa jina la AZAM TV.
Rais KIKWETE ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya habari na kusema kuwa serikali haina ugomvi na vyombo vya habari binafsi isipokuwa vinapaswa kuzingatia sheria za nchi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Rais pia amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo Kifo cha Mbunge wa MBINGA MAGHARIBI Marehemu Kapteni JOHN KOMBA pamoja na Maafa yaliyotokea KAHAMA mkoani SHINYANGA.
Uzinduzi huo imefanyika eneo la TABATA jijini DSM na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo DKT.FENELLA MUKANGARA pamoja na Naibu waziri wa FEDHA MWIGULU NCHEMBA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment