Image
Image

Rais Kikwete awatembelea wahanga wa Mafuriko 1500 wanaolala nje baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji Buguruni jijini dar leo


Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitizama namna ambavyo maji yametuama kwenye nyumba Buguruni kwa mnyamani  leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Na.Msaka Noti.

Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Buguruni Mnyamani ili kujionea madhara makubwa ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha zaidi ya watu 1500 kukosa hifadhi baada ya nyumba zao kuingiwa na maji.


Baada ya Rais Kikwete kuwasili  katika eneo hilo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es salaam huku akizingirwa na umati mkubwa wa watu,baadhi ya wakazi hao wamesikika wakipongeza ujio wa rais kufika katika eneo hilo ili kujionea walivyokimbia makazi yao baada ya maji  kuingia katika nyumba zao na kuwalazimu kulala nje wakilinda mali zao.


Akizungumza na wakazi wa Buguruni Mnyamani,Rais Kikwete amesema amelazimika kufika katika eneo hilo ili kuona jitihada zinazofanyika za kuondoa maji hayo ili wananchi wawe salama huku akikisisitiza kuwa baada ya maji hayo kuondolewa, ujenzi wa bomba mpya ambao ni mkubwa ufanyike ili kusaidia kupitisha maji wakati wa mafuriko.


Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo akiwemo mzee Saidi Mohamed Bakari amesema wanaishi maisha ya tabu na wana siku saba hawajalala kutokana na maji hayo kuingia ndani ya nyumba zao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment