Image
Image

Rais Obama arefusha vikwazo dhidi ya Robert Mugabe wa zimbabwe na watu wake

Rais BARACK OBAMA wa Marekani amerefusha vikwazo dhidi ya Rais ROBERT MUGABE wa Zimbabwe na watu wake wa karibu, huku serikali ya Uingereza ikimtuma Zimbabwe Waziri wake wa Maendeleo ya Kimataifa kwa ajili ya mazungumzo na utawala wa Nchi hiyo.
Chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF kimelaani hatua hiyo ya Rais wa Marekani ya kurefusha muda wa vikwazo dhidi ya Rais Mugabe na watu wake wa karibu.
Obama amesema kuwa tishio lililotokana na vitendo na sera za baadhi ya wanachama wa serikali ya Zimbabwe na watu wengine za kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia nchini humo bado lipo pale pale.
Amesema ni kutokana na sababu hiyo ndio maana ameona kuna umuhimu wa kuendeleza kwa nguvu vikwazo kwa Rais Mugabe na watu wake wa karibu ili wachukue hatua kuhusu suala hilo.
Katika hatua nyingine serikali ya Uingereza imethibitisha kuwa, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa nchi hiyo Bwana  MARK LOWCOCK wiki hii ataelekea Zimbabwe kwa ajili ya mazungumzo na Waziri wa Fedha na maafisa wengine wa nchi hiyo PATRICK CHINAMASA

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment