Image
Image

Rais Kikwete asema nchi wanachama wa EAC wanawajibu wa kupunguza tofauti na kuweka usawa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amesema kuwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wana wajibu wa kupunguza tofauti za usawa na kuongeza ushirikishaji wa maendeleo miongoni mwa nchi wanachama wa nchi hizo kama njia ya kuendeleza jumuiya hiyo.
Alisema kuwa hali ya baadaye ya jumuiya hiyo itategemea jinsi gani wananchi wa nchi wanachama wanavyohisi wananufaika na kuwepo kwa Jumuiya hiyo na uanachama wao.
Pia akawataka wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kushughulika na yale mambo ya Afrika Mashariki badala ya kila mbunge kushughulikia mambo ya nchi yake.
Rais aliyasema hayo Alhamisi wakati alipohutubia Bunge la Afrika Mashariki mwanzoni mwa kikao cha Bunge hilo katika Bunge la Burundi mjini Bujumbura, ambako alizungumzia hali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aliwaambia wabunge hao kuwa hali ya baadaye ya jumuiya itategemea jinsi nchi wanachama zinapunguza tofauti za usawa miongoni mwao na jinsi zinawashirikisha wananchi katika maendeleo ya pamoja.
“Sisi kama viongozi tusipolifanya hili, tutajikuta mahali ambako Jumuiya yetu inakufa tena, na kamwe hatutaki kuona Jumuiya hii inakufa kama ile ya zamani,” alisema na kuongeza; “Hali ya baadaye ya jumuiya itategemea jinsi sisi viongozi tunavyofanikiwa kuwafanya wananchi hao kujiona na kujisikia kama wananufaika na jumuiya yetu.
Na hili haliweza kufanikiwa kwa sisi viongozi kusema kuwa Jumuiya imefanikiwa. Ni lazima wananchi wayaone na wayahisi mafanikio hayo.” “Lazima muonekane mnatumia muda wenu mwingi kujadili na kufanya maamuzi kuhusu mambo yanayowahusu wananchi wa Afrika Mashariki na siyo vinginevyo. Lazima mtoe kipaumbele kwa mambo ambayo yanasura ya Afrika Mashariki kuliko mambo madogo madogo ya manufaa ya nchi zenu. Lazima tuone moyo wa uafrika mashariki ndani yenu na katika maamuzi yenu.”->>>http://www.habarileo.co.tz
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment