Image
Image

Rais wa ZAMBIA EDGAR LUNGU afanyiwa upasuaji wa koo akiwa nje ya Nchi

Habari kutoka nchini ZAMBIA, zinasema rais wan chi hiyo EDGAR LUNGU amefanyiwa upasuaji wa koo akiwa nje ya nchi alikolazimika kupelekwa baada ya kuugua ghafla.
Awali madaktari wanaotibu nchini humo walidau kuwa LUNGU alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Kiongozi huyo wa ZAMBIA aliyechaguliwa mwezi januari kuliongoza taifa hilo, alianguka na kuzimia jana jumapili, alipokuwa akitoa hotuba mjini LUSAKA, wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
LUNGU alikimbizwa hospitalini baada ya tukio, na madaktari wakaidhinisha kuwa apatiwe matibabu ya haraka nje ya nchi. Wakati wa kampeni za uchaguzi wapinzani walidai kuwa LUNGU mwenye umri wa miaka 58 ni mgonjwa, taarifa ambazo mwenyewe alizipinga.
Rais huyo wa ZAMBIA alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa rais wan chi hiyo MICHAEL SATA, kutokana na maradhi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment