Image
Image

Serikali imesema haina mpango wa kufanya marekebisho ya katiba ili kufanya Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupatikana kwa zamu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.




Serikali imesema haina mpango wa kufanya marekebisho ya katiba ili kufanya Marais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania kuweza kupatikana kwa zamu kati ya Tanzania bara na Zanzibar.
Naibu waziri wa sheria na katiba Ummy Mwalimu amesema kufanya hivyo ni sawa na kuzorotesha Demokrasia hapa nchini hivyo kamwe hakutakuwa na mpango wa kurekebisha katiba katika kipengele hicho.


Amesema kuruhusu kitendo hicho ni sawa na kuruhusu mgawanyiko katika nchi kwani katiba ya hivi sasa imetoa uhuru wa upande wowote kugombea nafasi ya Urais kama ana sifa kama zilivyoainishwa katika katiba ibara ya 39.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge mama Anna Makinda amekataa kuzungumzia lolote kama kutakuwepo au la muswada wa vyombo vya habari katika mkutano wa 19 wa bunge la Jamhuri ya Muungano linaloendelea mkoani Dodoma.

Spika Makinda amefanya hivyo kufuatia ombi la muongozo kutoka kwa mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo aliyetaka kujua kama muswada huo utakuwepo au la katika mkutano huu wa Bunge unaoendelea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment