Image
Image

Serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele kwa mpango wa BRN katika kutekeleza majukumu yake

Serikali imesema inaendelea kutoa kipaumbele kwa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa -BRN katika kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa ni ile yenye manufaa na ya haraka kwa wananchi wengi.
Akizindua taarifa ya mwaka ya matokeo ya utekelezaji wa mpango huo jijini DSM Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema mpango huo una uwezo wa kufanikisha mambo mengi kwa muda mfupi na kufikia malengo yaliyowekwa kwa haraka zaidi.
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ambao Serikali imezindua ripoti ya kwanza ya utekelezaji wake jijini DSM iliyoainisha mafaniko yaliyopatikana katika Sekta SITA za mwanzo za kipaumbele kwa mwaka 2013/2014.
Mbunifu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi -PDB OMAR ISSA amesema mfumo huo ni wa wazi ambao umeleta nidhamu katika utendaji kazi na kueleza ripoti hiyo kabla ya kuzinduliwa kampuni binafsi ilifanya uchunguzi na kugundua vilivyoelezwa kwenye ripoti hiyo ni kweli.
Mashuhuda wa BRN nao wakatoa ushuhuda wao jinsi mpango huo ulivyowasaidia hususan katika kupatiwa mafunzo yaliyoweza kubadilisha masuala mbalimbali ikiwemo kilimo na ufundishaji.
Mikakati hiyo ya BRN ilitekelezwa kwa mujibu wa Mpango kazi wa miaka mitatu ambao ulizinduliwa mwaka 2013.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment