Image
Image

Serikali ya TANZANIA kunufaika zaidi na msaada kutoka nchini CHINA

Serikali ya CHINA imesema itaongeza nguvu katika uhusiano wake na mataifa ya AFRIKA katika sekta kuu muhimu ikiwemo viwanda, afya na kuimarisha usalama na amani ambapo TANZANIA ni miongoni mwa nchi za AFRIKA ambazo tayari zimetiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo na nchi hiyo.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa CHINA, WANG YI katika mkutano na waandishi wa habari ukiwa ni mwendelezo wa mawaziri wa CHINA kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utendaji wa kazi za wizara zao katika kipindi hiki ambacho bunge la watu wa CHINA (NPC) likiendelea na vikao vyake.
waziri WANG LI anasema CHINA itaendelea na ushirikiano hususani kuyapa nguvu maendeleo ya viwanda, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kwa kujenga uwezo kwa waafrika kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yamlipuko ikiwa ni panoja na kusaidia bara la AFRIKA kudumisha amani na usalama kwa kujua nyenzo muhimu za kupamba na kukomesha makundi mbalimbali yakiwemo ya kigaidi na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
March 2013 wakati wa ziara ya rais wa CHINA XI JINPING nchini TANZANIA, serikali ya CHINA na TANZANIA zitiliana saini ya ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo, mawasiliano, nishati na miundombinu.
Aidha waziri WANGI LI amesema CHINA itaendelea na mchango wake kutoa misaada ya hali na mali katika kupambana na ugonjwa wa EBOLA unayoyakabili mataifa ya AFRIKA MAGHARIBI.
Tayari nchi ya CHINA imepeleka wataalamu 100 wa afya katika mataifa yaliyoathiriwa na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa dola za MAREKANI milioni 122 kwa mataifa hayo.
Mwezi uliopita CHINA iliteua mwakilishi wa kudumu katika umoja wa AFRIKA (AU) ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuimarisha mahusiano na bara la AFRIKA.
Mawaziri mbalimbali kutoka bara la AFRIKA na wale wa CHINA wanatarajia kukutana katika Mkutano wa sita kuhusu ushirikiano wa AFRIKA na CHINA (FOCAC) unatarajia kufanyika baadae mwaka huu nchini AFRIKA KUSINI.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment