Serikali wilayani Mufindi imeunda Kamati mbili ikiwemo ya uangalizi wa
mizigo ya abiria waliohusika kwenye ajali ya basi na lori iliyosababisha
watu 50 kupoteza maisha Wilayani Mufindi mkoani IRINGA, huku miili
AROBAINI na TISA iliyokuwa imehifadhiwa kwenye vyumba vya kuhifadhia
maiti katika hospitali za wilaya ya Mufindi na ile ya Rufaa tayari
imetambuliwa .
Mkuu wa Wilaya hiyo MBONI MUHITA amesema Kamati hiyo itahakikisha
kuwa mizigo ya abiria waliokuwa kwenye basi na ile ya kwenye lori
inakuwa salama hadi ndugu wa marehemu watakapofika kuitambua.
Kabla ya Kuunda kamati hiyo, Mkuu huyo wa wilaya akiongozana na
kamati ya Ulinzi na Usalama ikatembelea eneo la ajali na kutathmini
chanzo cha ajali hiyo ili kuchukua tahadhari zaidi kwa siku za badae.
Mhita anasema kamati nyingine ya Kuchunguza chazo halisi cha ajali hiyo itatoa tathimini yake baada ya uc hunguzi.
Katika hatua nyingine Mganga Mkuu wa mkoa wa Iringa Dokta Robert
Salim amesema kuwa miili 49 kati ya 50 iliyokuwa imehifadhiwa kwenye
vyumba vya kuhifadhia maiti katika hospitali za wilaya ya Mufindi na ile
ya Rufaa ya Iringa imekwishatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa
kwenda kuzikwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu Mwili mmoja uliobaki umetambuliwa kuwa ni
wa raia wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo ambaye unasubiri kuchukuliwa na
ndugu zake.
Hali za majeruhi wa ajali hiyo zinaendelea vizuri huku wale
waliolazwa Mufindi wakiruhusiwa wote huku majeruhi sita wakiendelea na
matibabu hospitali ya Rufaa Iringa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment