Image
Image

Taifa Stars yawasili salama jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames), mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini Mwanza.
Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.
MALAWI KUWASILI ALHAMISI
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.
Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).
Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).

VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ianatrajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kwa wenyeji JKT Ruvu kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo timu ya Young Africans.
KILUVYA BINGWA SDL
Timu ya Kiluvya United ya mkoa wa Pwani jana imetawazwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya kuifunga Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
Kiluvya United inaunganana timu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa, Katavi FC na Volcano zikishuka daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment