Image
Image

Vijana wavamia nyumbani kwa Mh.Lowassa kumshinikiza kuchukua fomu ilikugombea urais 2015


Rais wa serikali ya wanafunzi UDOM akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuandamana hadi nyumbani kwa Mh.Lowassa kumshinikiza kugombea urais mwaka huu.

Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.

Aidha Lowassa kwa Upande wake amewashukuru vijana hao na kusema kuwa ujio wao na ule wa masheikhe wa Bagamoyo unazidi kumhamasisha kutangaza nia na pindi muda ukifika anaweza kufanya hivyo.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais.
Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu. Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment