Taarifa ya UNHCR imemnukuu Bwana Guterres
akisema kuwa kufuatia janga hilo la kihistoria ametaka msada wa haraka wa uokozi
kwa manusura wa ajali hiyo huku pia akitaka pia suluhu la muda mrefu
la uhamiaji wa kwenda barani Ulaya.
UNHCR imesema inafanya uwakili ili kupata
mwitikio chanya kwa nchi za jumuiya ya Ulaya EU la kushughulikia changamoto
zinazowakabilina maelfu ya watu wanaohatarisha maisha yao kutafuta usalama na
maisha bora barani humo.
Katika kutatua tatizo la wahamiaji haramu
na wakimbizi wanakutw na sintofahamu, UNHCR imesema imeandaa mapendekezo
ikiwamo utafiti yakinifu, operesheni za uokoaji, utafuataji wa
makazi salama, vibali vya kusafiria kama sehemu ya usaidizi wa kibinadamu
pamoja na kuunganishwa tena na familia.
Kufikia mwaka 2015, zaidi ya watafuta
hifadhi 35,000 na wahamiaji wamewasili kwa njia ya boti barana Ulaya na ikiwa
idadi ya vifo katika ajali ya jumamosi vitathibitishwa itafikisha idadi ya 1600.
Mwaka 2014 takribani watu 219,000 walivuka Mediterranian na 3,500 walipoteza
maisha.
0 comments:
Post a Comment