Image
Image

Askofu Gwajima afikishwa mahakama ya kisutu na kusomewa mashitaka mawili yaanayomkabili ikiwemo la kutoa lugha ya matusi kwa Polycarp Kardinali Pengo.


Kiongozi mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima askofu Josephat Gwajima amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini dar es salaam na kusomewa mashitaka mawili yanayomkabili ikiwemo kutoa lugha ya matusi dhidi ya  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akisomewa mashtaka wawili yanayomkabili na mawakili waandamizi wa serikali kwa  upande wa jamuhuri ambao ni shadrack kimaro na tumaini kweka, mbele hakimu wilfred dyansobera,wamesema askofu josephat gwajima alitenda kosa la kwanza la kutoa lugha ya matusi akiwa katika viwanja vya tanganyika peakers kawe jijini dar es salaam dhidi askofu mkuu wa kanisala katoliki cardinary pengo huko kosa la pili ikiwa ni kushindwa kuhifadhi silaha pamoja na risasi wakati akiwa katika hospitali ya tmj jijini Dar es salaam kinyume na sheria za silaha za moto.
Baada ya hakimu mh wilfred dyansobera kusikiliza pande zote ikiwemo upande wa jamhuri na upande wa mlalamikiwa,katika makosa yote mawili, baada ya wakili wa askofu gwajima Dr.PeterKibatala kuoomba mahakama kumuachia mteja wake kwa dhamana,mahakama iliridhia na kumuachia huru askofu Gwajima kwa dhamana ambapo katika kosa la kwanza amejidhamini mwenyewe kwa kutoa shilingi milioni moja na katika kosa ya pili ametolewa na dhamana ambapo baada ya mahaka kumuachia huru pamoja na baadhi ya wafuasi wake  watatu walikamatwa na kufikishwa mahakamani hapo.
Kabla ya hapo ITV ilishuhudia askari wa jeshi la polisi wakiwa wamezingira geti la askofi Gwajima nyumbani kwake salasala hali iliyotia hofu kwa wakazi wa maeneo hayo na viongozi wa maeneo hayo kama anavyoeleza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kilimahewa kata ya wazo alipojengwa askofu Gwajima.
Baada ya askari wa jeshi la polisi kuondoa katika nyumba ya skofu Gwajima ,umati ya waumini wake walimiminika nyumbani kwake ambapo baada ya muda mfupi alioondoka kwenda katika kituo kikuu cha polisi CENTRAL ambapo baada ya kuingia ndani na kukaa kama dakika 10 aliondolewa chini ya ulinzi na kufikishwa katika mahakama ya hakimu kisutu.
Baada ya kuachiwa huru waumini wake waliofika mahakamani hapo walianza kuimba nyimbo ambapo kwa mujibu wa wakili wa askafu Gwajima anatakiwa kupanda kizimbani tena tarehe 4 mwezi may 2015 akiongozana na wafuasi wake walioshtakiwa.
Chanzo ITV

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment