Balozi wa Malawi nchini Mhe. Hawa Ndilowe ameyasema hayo jijini Dar es salaam
alipomtembelea ofisini kwake Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini – TPSF Dr.
Reginald Mengi.
Kauli ya Balozi huyo inatokana na ushauri wa Dr. Mengi kuwa Wafanyabiashara wa Tanzania na
Malawi hawana budi kushirikiana katika biashara za ubia ili kujiimarisha kiuchumi
na kudumisha ujirani mwema, na kusisitiza kuwa
ili uwe endelevu, ushirikiano huo ujadiliwe katika ngazi ya uongozi wa Taasisi
za sekta binafsi:…
Dr. Mengi pia amezishauri nchi za Afrika kufanya
biashara baina yao kwa kuacha kasumba ya kupenda kuagiza bidhaa kutoka nje ya bara hili.
Pia amezishauri nchi za Afrika kuwawezesha wananchi
wake kudhibiti na kumiliki uchumi wa nchi ili kudumisha amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment