Image
Image

Breaking News: Watu 9 waliokuwa wamejifungia msikitini wakiwa na vifaa vya milipuko na silaha wakamatwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro



Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watu tisa   wakiwa na silaha za kulipua na nguo za jeshi la wananchi  wakiwa wamejifungia katika  msikiti  wa Suni  Kidatu  wilayani   kilombero  mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi  mkoa wa Morogoro lenard Paul amesema tukio la kukamatwa kwa watu hao  limekuja kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu ambapo  jambazi mmoja aliruka katika bajaji na kisha kumjeruhi  askari  shingoni  ambapo  wananchi wenye hasira kali  walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza  jambazi huyo akiwa na silaha  na kisha  kumchoma moto.

Kamanda Paul amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliongeza nguvu  ya  askari ambapo walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine  wakiwa katika msikiti wa Suni Kidatu na baada ya kupekuliwa wamekutwa na vifaa vya Milipuko,Nguo za jeshi la wananchi (JWTZ) ambapo jeshi hilo linaendelea kuwashikilia watuhumiwa na  kunataarifa kuwa watuhumiwa hao walijiandaa kufanya tukio la uhalifu.

Aidha kamanda Paul amewashukuru wananchi wa Ruhembe Kidatu wilayani kilomeroa mbao wametoa ushikiano kufanikisha kukamtwa kwa watuhumiwa hao.  

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment