Watu 19 wamefariki dunia baada ya Hiace waliokuwa
wakisafiria kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kiwira wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Miili
ya watu kumi na tisa waliofariki dunia ikiwa inaonekana imelazwa chini hapo
huku ndugu jamaa na mashuhuda wakiangalia namna hali ilivyokuwa.
Watu 19 kati yao 17 wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa baada
ya gari dogo la kusafirisha abiria aina ya toyota Hiace kushindwa kukata kona
kali katika eneo la Kiwira wilayani Rungwe na kupinduka kabla ya
kutumbukia mtoni.
Gari hilo lenye namba za usaji T290 ABU ambalo
limesajiliwa kufanya safari zake kama daladala jijini mbeya, leo asubuhi
limepakia abiria wapatao 20 kwa ajili kuwasafirisha kwenda tukuyu wilani Rungwe
na likiwa katika mwendo mkali dereva wake ameshindwa kukata kona kali za
ilongobota, eneo lijulikanalo maarufu kwa jina la uwanja wa ndege na kutumbukia
katika mto kiwira kama ambavyo baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wanavyoeleza.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya rungwe Dk. Aminiel
Ngumuo amekiri kupokea miili 17 ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya
ya Rungwe,makandana na majeruhi watatu ambao wanatibiwa katika
hospitali ya misheni ya igogwe ambako pia mwili majeruhi aliyefariki wakati
akipelekwa hospitalini hapo umehifadhiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo chake ni mwendo kasi, huku akiwata
madereva kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
0 comments:
Post a Comment