Hayo
yamebainishwa na katibu wa chama cha kutetea abiria chakua Bwana Godwin Mtongeji
jijini dar es salaam na kueleza kuwa sababu zilizotolewa na SUMATRA za
kushindwa kushusha nauli kwa kigezo cha usumbufu wa chenji haina mashiko na
imeangalia upande mmoja wa wamiliki wa daladala huku wakieleza kushangazwa na
nauli za mikoani kushuka kwa kiwango kidogo sana ambapo kwa baadhi ya ruti za
mikoani unakuta tofauti ya nauli za sasa na zazamani ni kati ya 1800 mpaka
3000.
TAMBARARE HALISI ilipata nafasi ya kupita
katika baadhi ya vituo mbali mbali vya
daladala jijini dar es salaam kusikia nini maoni ya wakazi wa jiji hilo juu ya
swala hili la nauli?. ambao baadhi yao wameeleza kutotendewa haki na SUMATRA
kutokana na kutoshuka kwa nauli hizo jambo linalowapa wasiwasi wa uwepo wa
maslahi binafsi katika kuamua maswala haya ya kushusha nauli na kusababisha
kutowatetea wananchi wa hali ya chini ambao ndiyo wanaotakiwa kuangaliwa sana.
Wamesema
ipo haja yakuona kuwa wananchi kipato wanachokipata nikidogo mno ambapo hali ya
uchumi nayo inaonekana kuyumba hivyo ingekuwa jambo la busara kwa SUMATRA kuona
kunahaja ya ushushaji wa nauli kwa dala dala jijini na ikizingatiwa kwa upande
wa vijana hali si shwari kwakuwa hawana kazi za kuaminika za kuwaingizia kipato
licha ya pesa wanayoipata hutumika nauli na kula jambo ambalo linawafanya
kusonga mbele kiuchumi.
Nisiku
ya pilio leo tangu mamlaka ya uthibiti
wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA kutangaza viwango vipya ya nauli vitakavyoanza kutumika
april 30 mwaka huu ambapo nauli za mabasi ya mikoani ndizo zilizoshushwa kwa
asilimia 7.8 na kuziacha nauli za daladala zikiwa zilezile kwa madai kuwa
katika ukokotoaji ili kushusha nauli za dala dala imeshindikana.
0 comments:
Post a Comment