Hayo yamebainika na mkuu wa
kitengo cha upasuaji wa moyo Dk. Evarest Nyawawa wakati wa ufunguzi wa mashine
ya ya uchunguzi wa mishipa ya moyo na kuzibua mishipa ya iliyoziba kwenye moyo
na kuweka kifaa maluum kiitwacho STENT ili kuruhusu damu kuendelea kusukumwa
ambapo amesema kwa wagonjwa wa mijini maradhi hayo yanatokana na ukosefu wa
mazoezi na ulaji mbaya usiozingatia lishe bora.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya
tiba na upasuaji moyo Prof. Mohamed Janabi amesema dhana ya kuongeza
ushirikiano na nchi nyingine ni kuboresha huduma za upasuaji wa moyo ambapo
kutokana na kuwepo na kifaa hicho sasa muhimbili kupitia kitengo cha moyo
inaweza kupokea wagonjwa kutoka jumuiya ya afrika mashariki nakuongeza kuwa kwa
kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuwafanyia upasuaji wa moyo wagonjwa.
Mmoja wa madaktari kutoka india
ambaye anashirikiana na madaktari kutoka marekani ambao wameletwa na serikali kufanya upasuaji huo na kuwafundisha
madakatari wa hapa nyumbani ameeleza tatizo hilo linawakumba sana nchi
zinazoendelea huku daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa hospitali ya muhimbili
akieleza kuwa mashine hiyo itaokoa gharama kubwa serikali iliyokuwa inatumia
kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambapo mgonjwa mmoja wakati mwingine alikuwa
anatumia zaidi ya milioni 20.
0 comments:
Post a Comment