Image
Image

Kutokutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa wakati stahiki imechangia wanandoa kushindwa kutumia uzazi wa mpango.


Jamii imekuwa haipati elimu ya afya ya uzazi kwa uhakika nchini,hali inayosababisha kiwango cha watu wengi walioko kwenye ndoa kushindwa kutumia uzazi wa mpango kupanda hadi asilimia 25 kutoka asilimia 23 ilivyokuwa awali .
Kutokana na hali hiyo, wasichana  zaidi ya  Elfu-8 hupoteza haki yao ya kupata Elimu kwa kupata mimba zisizotarajiwa, na pia kuchangia ongezeko kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Marie Stopes ,Bi ELLY REWETA ameyasema hayo Mjini Mpanda Mkoani Katavi, wakati shirika hilo lilipokuwa likizindua rasmi huduma za uzazi wa mpango kwenye mkoa huo .
Amesema  wanawake 255 kati ya  kila   wanawake  Laki-Moja   h upoteza maisha kila mwaka kwa ajili ya uzazi, na wengi wakijifungulia majumbani kwa zaidi ya asilimia 60, na kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuifikisha eli mu hiyo ya afya ya uzazi hadi  shuleni ili kuwaokoa vijana wengi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ,Bwana  PAZA MWAMLIMA, akimwakilisha mkuu wa mkoa huo wa Katavi ,   Dakta IBRAHIM MSENGI katika uzinduzi huo, ametoa wito kwa jamii ya mkoa huo kutumia kwa dhati huduma za uzazi wa mpango zinazotolewa na Marie Stopes .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment