Image
Image

Maalim Seif atinga mahakama ya kisutu kumdhamini Prof.Lipumba na wafuasi wake kufuatia kufanya mkusanyiko na maandamano, kinyume cha sheria.





Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad,amefika katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini dar es salaam kufuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim lipumba na wafuasi 29 wa chama hicho wanaotuhumiwa kutenda makosa matatu,ikiwamo kufanya mkusanyiko na maandamano, kinyume cha sheria.

Maalim Seif, ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ amelakiwa na Prof. Lipumba na mamia wa wafuasi wa chama hicho waliofika katika mahakama hiyo kufuatilia kesi hiyo pamoja na kuwadhamini wafuasi wenzao.
Wakili wa upande wa jamhuri, amewasomea mashtaka washtakiwa wawili kati ya 30, ambao ni Shhaweji Mketo na Hemed Abdallah, ambapo wanakabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kufanya mkusanyiko usio halali na maandamano, kinyume cha sheria.
Mashtaka mengine, wanayotuhumiwa nayo ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa na kufanya fujo, kinyume cha tamko la polisi lililowazuia kukusanyika na kuandamana.
Wanatuhumiwa kutenda makosa hayo maeneo ya mbagala, jijini dar es salaam ambapo wote walikana makosa hayo na wako nje kwa dhamana hadi mei 6, mwaka huu kesi yao itakapokuja kwa ajili ya usikilizaji wa awali.
Watuhumiwa wengine 20 pia walipata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana na usikilizaji wa awali wa kesi yao utafanyika mei 6, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, maalim Seif aliwashukuru wafuasi wa chama chake, kujitokeza kwa wingi na waliowadhamini watuhumiwa akisema hiyo inaashiria kuwa tatizo linalowakabili wenzao siyo lao peke yao, bali ni la wote.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment