Image
Image

Makada wa chama cha mapinduzi CCM mkoani arusha wakitabiria vibaya chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini baadaye mwaka huu.


Baadhi ya makada wa Chama  cha Mapinduzi  Mkoani  Arusha  wamesema  usaliti , majungu  na unafiki  unaoendelea  ndani ya  chama  hicho visipodhibitiwa ,chama hicho  kitaendelea  kushindwa  katika chaguzi   zinazotarajiwa  kufanyika  katika  maeneo mbalimbali  ya mkoa  huo .
Wakizungumza  wakati  wa kumsimika  Kamanda  wa vijana  wa Kata  ya Sombetini , Bwana BAKARI  MSANGI ,makada  hao wamesema  inasikitisha kuona  hata viongozi  wa juu  wanawajua  watu  wanaokisaliti  chama ,lakini  hawachukui  hatua badala yake wanabaki   kulalamika .

Akizungumzia malalamiko hayo  Mwenyekiti  wa  Chama cha Mapinduzi    wa  Wilaya ya  Arusha,Bwana WILFRED  SOILELI ,pamoja na  kukiri  kuwepo  kwa makundi  yanayotajwa  kuwa  yanakihujumu  chama ,   amewataka  watajwe  hadharani  ili  wachukuliwe  hatua .

Kwa  upande  wake  kamanda  wa  vijana  aliyesimikwa   Bwana  BAKARI  RAHIBU MSANGI  amewa taka  vijana  kuwa  wa kwanza kupambana  na  watu   wanaokisaliti  chama  na  kutowafumbia  macho  baadhi ya watu  wanaofanya  vitendo  hivyo .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment