Image
Image

Mamalishe jijini Arusha wapo hatarini kukubwa na magonjwa ya milipuko kutokana na uchafu uliokithiri eneo hilo wanapofanyia biashara zao.



Wananchi wa jijila Arusha wakiwemo wanaoendesha shughuli zao katika masoko likiwemo la  kilombero wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na kukithiri kwa  uchafu unaotokana na kutowajibika kwa watendaji wenye dhamana ya kusimamia usafi   
Baadhi ya wanachi wanaokabiliwa na tishio hilo wakiwemo mama lishe wamemweleza mkuu wa  wilaya ya arusha Bw. Christopher Kangoe kuwa wanapowauliza watendaji wa sekta ya afya  juu ya tatizo hilo  wawajibu kuwa serikali haina fedha.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw.Juma Iddy amesema ameshapokea malalamiko ya tuhuma za  watendaji hao na kwamba hatua zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao sambamba na  kushughulikia tatizo la msingi.
Akizungumza na watendaji wote wa wilaya ya arusha mkuu wa wilaya Bw.Christopher  Kaangoye amesema kama kuna  mtendaji anayedhani  kuwa  hawezi kutimiza wajibu wake ni bora akaondoka kwani hali iliyopo haivumiliki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment