Image
Image

News Alert: Mashirika na watanzania wameombwa kuwa na utamaduni wa kuchangia shule maalumu za walemavu wangozi ili kuwanusuru na matukio yanayo wakumba ya kukatwa viungo na kuuawa.


Mashirika mbalimbali na watanzania kwa pamoja wameombwa kuwa na utamaduni wa kuchangia  na kuboresha shule maalumu ambazo zina walemavu wa ngozi ,badala ya kusubiri matukio ya uvamizi kutokea na kuanza kuchukuwa hatu ,kwa kufanya hivyo kuta saidia walemavu  wa ngozi kupata elimu bila ya kuwa na wasiwasi ya kuvamiwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent  Kone amesema hayo katika hotuba yake iliyo somwa na mkuu wa wilaya ya Singida, Bwana  Said Amanzi katika  hafla ya kukabidhi mradi wa uboreshaji wa miundombinu rafiki kutoka shirika la Koica  la nchini korea,na kusema kuwa mashirika kutoka  mataifa  mengine wame weza kuchangia na sisi watanzania   inatubidi  kuchangia kwani jukumu la kuwalinda walemavu wangozi ni ni la watanzai wenyewe na kuhakikisha wana pata  ulinzi na elimu kama watu wengine.

Kwa upande wake  meneja mradi wa kujitolea kutoka shirika la Koica nchini korea  Bi. Park Jieun amesema mradi wa uboreshaji  wa miundombinu katika chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu sabasaba umegarimu zaidi ya shilingi  milioni arobaini na mbili kwa ajili ya kuboresha mazingira ya chuo kwa kujenga mabweni,matanki ya maji na kuwasaidi walemavu  ili waweze kuishi kama watu wengi ambao siyo walemavu.

Awali  mkuu wa  chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu   cha sabasaba Bi. Fatuma Malenga ameiomba serekali kuangali uwezekano wa kukijengea uzio chuo na kuweka  vivuko maalumu pamoja na  alama  katika barabara ambayo ipo karibu na chuo  ili kuwawezesha wenye ulemavu wa ngozi  na  walemavu wengine kuishi katika mazigira salama.

Akishukuru Bi.Jo Yunsil Chilly kutoka shirika la Koica ambaye alikuwa akisimamia ujenzi wa mabweni na miundo mbinu ya maji  amesema kila mtu mwenye ulemavu ana haki sawa kama wengine wasio kuwa walemavu kwa kupata elimu,kazi na kuwa na maisha kama watu wengine,pamoja na jitihada walizo toa katika chuo hicho wana amini kuwa  zita wasaidia wananchi  kuongeza utoaji wa elimu kwa  walemavu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment