Image
Image

News Alert: Mkemia mkuu wa serikali asema sheria ya matumizi ya kemikali imetungiwa kanuni mpya ili kudhibiti matukio ya uhalifu katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Mkemia mkuu wa serikali,Prof. Samwel Manyele amesema sheria ya matumizi ya kemikali ya mwaka 2003 imefanyiwa marekebisho kwa kutungiwa kanuni mpya ili kudhibiti matumizi ya kemikali nchini na kukabiliana na matukio ya watu kumwagiwa tindikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Mkemia mkuu wa serikali, Prof. Manyele ameyasema hayo jijini mbeya wakati akikabidhi vyeti vya usajili wa muda kwa wasafirishaji,wauzaji na wasambazaji wa kemikali za aina mbalimali mkoani mbeya.

Baadhi ya wasafirishaji,wauzaj na wasambazaji wa kemikali mkoani mbeya wamesema hatua ya wao kupewa vyeti hivyo imewafurahisha kwa kuwa sasa watafanya kazi hiyo wakiwa huru na kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.

Katika miaka ya hivi karibuni,kemikali zimekuwa zikitumika vibaya kwa kuwepo matukio ya watu kumwagiwa tindikali, na kusababishiwa madhara makubwa, hali ambayo imeilazimu serikali kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment