Image
Image

News Alert: Mkurugenzi mtendaji TRL asimamishwa kazi kwa tuhuma za malipo kinyume cha mkataba

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Reli  nchini(TRL),Mhandisi Kapallo Kisamfu  amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa  malipo ya Sh. Bilioni 230 ya mabehewa ya Mizigo  yenye kasoro pamoja na kufanya malipo ya mabehewa yote kabla ya kukamilika.
Akitangaza maamuzi hayo ya kusimimishwa kwa  Mkurugenzi huyo leo jijini Dar es Salaam baada ya  ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi (ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema ameshtushwa  na malipo hayo kwani yamekiuka manunuzi ya  umma kwani mkataba wake ulikuwa TRL ilipe  nusu ya asilimia 50 lakini matokeo yake  mabehewa yamelipwa yote.
Amesema mabehewa 120 yaliyofika nchini yakiwa  yana kasoro aliyazuia baada ya kubaini hivyo n lakini TRL ilikuwa imeshalipa fedha yote katika  mazingira hayo yanaonyesha mkataba una dalili  ya hujuma.
Waliosimamishwa wengine ni Mhandisi Mkuu wa  Mitambo TRL,Ngosomwile Ngosomiles,Mhasibu  Mkuu,Mbaraka Mchopa ,Mkaguzi Mkuu wa Ndani  Jasper Kisiraga pamoja na Meneja Mkuu  Ferdinand Soka.
Kamati ya uchunguzi kwa watendaji hao kwa  kuidhinishwa kwa kulipwa kwa mabilioni ya  Shilingi itaongozwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali (CAG),Taasisi ya Kupambana  na Rushwa (Takukuru),Mamlaka ya udhibiti wa  Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),pamoja na  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza  na waandishi wa habari kuhusiana  kuwasimamisha baadhi ya watendaji wakuu wa kampuni ya Reli hapa nchini uliofanyika katika  ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment