Mkutano huu ambao
unafanyika kwa siku mbili tarehe 16-17 April 2015, una lenga kusikiliza kero za
wafanya biashara wanaotumia mpaka huu, kwani mpaka huu wa mtukula ni moja wapo
ya mpaka ambao umekuwa gumzo kwa wafanya biashara kutoka Uganda kuja Tanzania
au kutoka Tanzania kwenda nchini Uganda.
Moja wapo ya matatizo
makubwa yaliyopo ni utitiri wa vizuizi vya barabarani kwani kwa mfano halisi,
kutoka mtukula hadi Bukoba vipo vizuizi vya barabarani maarufu kama BERIA 7
ambapo mtukula penyewe zipo beria 3 moja ikisimamiwa na TRA, ya pili
ikisimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya Missenyi na ya tatu ikisimamiwa na
Jeshi la Polisi. Kyaka zipo beria 3.
Hata hivyo, mkoa wa
Kagera unaongoza kwa kuwa na vizuizi vya barabarani (beria ) jambo ambao
linatia hofu hata kisaikolojia kwanini uwepo wa vizuzi hivi. Waweza kufikiri
kuwa ni kwa sababu ya kulinda usalama wa wananchi au wasafiri na mali zao, na
pengine baadhu hufikiri kuwa na vizuzi vingi barabarani kunachochea ukuaji wa
biashara!
Mkutano umehudhuria na
wajumbe kutoka umoja wa Afrika Mashariki, wa Uganda na Tanzania. Baada ya
mkutano huu wa Mtukula, mkutano mwingine utafanyika katika mpaka wa Sirari/
Isebania , katika mpaka wa Uganda na Kenya
Katika mkutano huo,
Wafanyabiashara na wajasriamali
wanaofanya shughuli za
kibiashara katika mpaka
wa Mtukula unaounganisha
nchi ya Tanzania
na Uganda wameomba
mamlaka zinazohusika kuondoa urasimu na
vikwazo visivyo vya
kiforodha ili kuwaondolea
usumbufu kwenye shughuli
zao za kila
siku.
Wito huo
umetolewa na wafanyabiashara na wajasriamali
hao katika semina
iliyofanyika katika ukumbi
wa jengo la
Afrika Masharika liliopo Mtukula
wamesema kuwa kuna
vikwazo visivyokuwa vya
kiforodha katika protoko
ya soko la
Afrika Mashariki vinasababisha
kuwaingizia hasara wajasriamali
kwani hata biadhaa
zao hurabika na
kupoteza thamani wakati
wanatumia gharama kuzitafuta
na kuzizalisha.
Mjasiriamali Kasongo Kitwana Mirambo
kutoka mkoani Tabora
amesema kuwa amelazimika kuishia
mpakani na lengo
lake lilikuwa auze
karanga zake tani
kumi nchini Uganda lakini
ameshindwa baada ya kuwepo
vikwazo ambavyo katika
maelezo na protoko
ya soko la
Afrika Mashariki havijaainishwa kwenye
sheria hivyo vimemsababishia hasara
kubwa na kumwalibia malengo
yake.
Pia amelalamikia ushuru unaotozwa
kwenye bidhaa zinazosafirishwa akitolea
mfano kuwa wakati anatokea mkoani
Tabora alilipia ushuru wa
mazao lakini alitozwa tena
ushuru wa mazao
alipofika Mtukula na kuongeza
kuwa huko ni kumukandamiza mjasriamali
na hawezi kupata
faida na kufaidi
uwepo wa soko
la pamoja la
jumuia ya Afrika mashariki.
Ibrahimu Sekwaro
ambaye ni mmiliki
wa shule ya
Lake View iliyopo Bukoba
amesema kuwa kwa Tanzania
kuna mlolongo mrefu
unaoleta usumbufu kwa
wataalamu kama walimu wanaotaka kuja
nchini kufundisha kutoka nchi jirani
ambazo ni mwanachama
wa Jumuia mashariki
wakati protoko ya
soko la pamoja
limeelekeza watu wenye
ujuzi na kazi
ataweza kuajiriwa bila
vikwazo.
Amesema wakati
nchi nyingine mwanachama wakitoa
fursa hiyo kwa
unafuu hali ni
tofauti Tanzania ambapo
mtu anayetaka ajira
hiyo hulazimika kutafuta
kibali cha ajira
na vinapatikana kwa gharama
ya juu zaidi na
kupitia wizara tatu
tofauti mfano wizara
ya mambo ya
ndani,wizara ya Elimu
na mafunzo ya
ufundi na wizara
ya kazi hali
inayochangia kukosa
wataalamu wakati nchi
nyingine zikifaidika na
soko la pamoja la
jumuia ya Afrika mashariki.
Sekwaro pia ametolea
mfano wa ushuru wa
kodi ya forodha unaotozwa kwenye karatasi
zinazoagizwa kutoka nchi
mwanachama katika Jumuia
ya Afrika Mashariki
Kenya kuwa zipo
juu sana na
wakati nchi ya
Uganda inatoza ushuru
nafuu na kuwezesha
upatikanaji rahisi wa
bidhaa hiyo.
Kwa upande
wake Rwechungura Mali
ambaye ni Afisa Mtendaji wa chama
cha wafanyabiashara mkoa
wa Kagera TCCIA
amesema kuwa kuna
vikwazo vingi katika
mpaka wa Mtukula
na kuna baadhi
ya watendaji wa
Chakula na Dawa TFDA ,Kilimo na
wengineo wanafanya ubadilifu
walipisha wafanyabiashara ushuru
lakini hawatoi stakabadhi
za malipo.
Wakichangia mjadala
Afisa wa Mamlaka
ya Mapato amesema
kuwa wanatoza ushuru
kwa kufuata mwongozo
wa jumuia ya
Afrika Mashariki jibu
ambalo halikuweza kukidhi kiu
ya wafanyabiashara na
wajasrimali waliohudhuria semina
hiyo.
Hata hivyo wajasriamali wametakiwa kufuata
taratibu na kanuni
za kuwa na
vibali husika ili
kuepusha kutapeliwa na
kupata hasara kwa
kukosa utambulisho halali
wanapokuwa nchi nyingine za
jumuia.
Semina ya
hii imewezeshwa na
mwezeshaji toka nchini
Rwanda Christine Mukangoboka, wengine ni Robi
Ernest Bwiru kutoka
katika wizara ya
Afrika ya Mashariki nchini
Tanzania na wengine
ni maafisa kutoka
makao makuu ya
jumuia ya Afrika
Mashariki Arusha na wengine
kutoka wizarani nchini Uganda.
JUHUDI fELIX 0756
601054 Chanzo:Fadeco
0 comments:
Post a Comment