Mkuu wa mkoa wa kigoma
Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewaongoza mamia ya wakazi wa
manispaa ya kigoma ujiji kuaga miili ya watu wanane wakiwemo
wanafunzi sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya kibirizi
mjini kigoma walio fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua
iliyonyesha kwa takriban masaa matatu.
Akitoa salam za
rambirambi mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka
wafiwa na wananchi kuchukulia tatizo hilo kama ni tukio la ajali ya
kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.
Majonzi yalitawala
shughuli hiyo hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika viwanja vya shule
ya msingi kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari kwa maziko huku mwili wa
Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda moshi kwa maziko .
Kwa upande wao viongozi
wa dini Shekh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa
la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba huo, wamewataka waumini wa dini
mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila mwanadamu ataonja mauti kwa
wakati wake na kwamba imani za kishirikina zisihusishwe katika msiba huo.
0 comments:
Post a Comment