Image
Image

Mtu mmoja afariki kwa kugongwa vibaya na treni wakati akivuka reli mkoani Morogoro.



Mtu mmoja  amefariki    dunia   baada ya kugongwa vibaya  na  treni  wakati akivuka  reli  na kisha viungo vyake kusambaa  katika mtaa wa  ujenzi  manispaa ya morogor.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alijulikana kwa jina moja  la mangi ambapo  wameeleza  kusikitishwa na ajali kwakua  hii ni mara ya  tatu watu kugongwa na treni  katika maeneo hayo na kueleza kuwa   amarehemu alikua  anavuka  Reli.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa ujenzi Christopha Chales ameelezea  tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kupita kwenye njia ya Reli kwani wataendelea kusababisha ajali  zisizo za lazima  ambazo zingeweza kuepukika.

Askari wajeshi la polisi wamefika katika eneo la tukio  na  kuchukua mwili  wa marehemu ambapo umehifadhiwa katika  chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment