Image
Image

News Alert: Nchemba abainisha sababu kuu nne za msingi zinzofanya wananchi kumpendekeza kugombea urais mwaka huu.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amebainisha sababu nne zinazowafanya wananchi wampendekeze kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. 
Nchemba aliyasema hayo  kwenye mahojiano wakati wa kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV kuhusu tafiti zinazofanywa juu ya kukubalika kwa baadhi ya watia nia ya urais miongoni mwa wananchi wanaomtaja.  
“Nisingependa kuwa refarii na mchezaji kwa wakati mmoja katika hili. Kuna ripoti iliwahi kuonyesha kuwa ninaongoza katika mbio hizo kwa kupata asilimia 37 na nyingine ikasema nimeshika nafasi ya pili. Ninawashukuru wananchi wanaoona kuwa nafaa katika nafasi hiyo.”
Aliongeza: “Wanaonipigia kura wanaona nidhamu katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, matumizi. Pia mabadiliko ya kukomesha ufanyaji kazi wa mazoea.”
Tangu ateuliwe kushika wadhifa wa Unaibu Waziri, Nchemba alisema amefanya mabadiliko kadhaa ambayo yamesaidia kudhibiti matumizi ya Serikali, ikiwamo kupitisha malipo ya wafanyakazi wote wa serikali katika akaunti zao za benki. 
Sambamba na hilo aliagiza wakuu wa idara wote kuhakiki taarifa za watumishi walionao katika ofisi zao jambo lililochangia kuokoa zaidi ya Sh400 milioni zilizokuwa zinalipwa kwa waajiriwa hewa.
Pamoja na hayo alisema kuwa, kwa sasa amejikita zaidi katika kutekeleza majukumu yake ya unaibu waziri.
Alipoulizwa anachukuliaje kufananishwa na aliyewahi kuwa waziri mkuu katika utawala wa awamu ya kwanza, Edward Sokoine, alijibu kuwa hiyo ni ishara nzuri kwani kiongozi huyo alitukuka katika utumishi wa umma.
“Hilo linanifanya nitende kulingana na mahitaji ya wananchi. Uongozi wa Sokoine ulipendwa na wengi na kufananishwa na kiongozi aliyetukuka kama yeye ni sifa nzuri inayoniongezea ari,” alisema.
Kuhusu kuvaa viatu vyake, Sokoine alibainisha kuwa hilo bado kwani nafasi anayohudumu hailingani na ile aliyokuwa nayo Sokoine.
Akizungumzia mtindo wake wa kuvaa skafu ya bendera ya Taifa alisema, anatazamia kuwa baada ya muda mfupi itakuwa ni utambulisho wa taifa kwa kila Mtanzania atakayeenda nje ya nchi.
“Nilianza kuvaa skafu tangu nikiwa sekondari…wakati huo zenye rangi za bendera ya taifa hazikuwa nyingi lakini kadri siku zinavyosogea zinaongezeka.
Viongozi wakubwa Afrika walikuwa na mavazi yaliyowatambulisha,” alisema akitolea mfano marais Keneth Kaunda wa Zambia na Kwame Nkurumah wa Ghana.
Akifafanua kuhusu mpango wa Serikali kuongeza mapato na migomo ya wafanyabiashara ya mara kwa mara inayoendelea alisema kuwa inachafua sifa nzuri ya Taifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment