Akitoa
hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Tabora mjini, Mhe. Bahati Chitepo
amesema kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia
kama hiyo kwa watoto, na jamii ijifunze kutoka kwake.
Awali
mwendesha mashitaka wakili wa serikali bw. Miradi kijulu amesema kuwa,
mshitakiwa (MASOUD NASORO) alitenda kosa hilo eneo la kata ya kiloleni ambapo
muathirika wa tukio hilo alimuomba lifti akiwa anakwenda shuleni na ndipo
mshitakiwa alimpeleka vichakani mtoto huyo eneo la kalunde na
kumfanyia unyama huo.
Baada
ya kutenda kosa hilo mshitakiwa alikimbia hadi alipotiwa nguvuni na jeshi la polisi
na kufikishwa mahakamani,hata hivyo mshitakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo
impunguzie adhabu kwani anaishi na babu yake mlemavu wa mguu na wazazi wake
wote wamafariki dunia, maombi ambayo yaliyupiliwa mbali.
0 comments:
Post a Comment