Akizunguza na Mhe. Ali Ahmed
Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman siku ya Alhamis tarehe 16 Aprili 2015,
Waziri Membe amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa Watanzania hao
ambao wengi wao ni wanafunzi, wanarejea nyumbani salama.
Zoezi la kurudisha Watanzania
hao lilianza siku chache zilizopita ambapo familia ya watu watano ilisaidiwa na
kurudi nyumbani kupitia Oman, wakati zoezi la kuwatambua na kuwaandikisha
Watanzania likenddelea.
“Nimeruhusu matumizi ya fedha
ya dharura ili kuhakikisha ndugu zetu walioko kwenye hatari na machafuko ya
Yemen wanarejeshwa salama nyumbani mara moja” alisema Mhe. Membe.
Watanzania hao ambao wengi wao
hadi sasa wameshafika kwenye miji midogo ya Sarfat na Al-Mazyouna kwenye mkoa
wa Salala mpakani mwa Oman na Yemen, walituma maombi ya dharura (distress call)
kwenye Ofisi za Ubalozi Oman, kuelezea mazingira ya hatari yanayowakabili, na
kuomba kurudishwa nyumbani.
“Kulingana na maelekezo ya
Waziri Membe, zoezi la kuwarejesha Watanzania limeanza. Nimewapeleka maafisa wa
ubalozi kule Salala ni kilometa takriban elfu moja kutoka Muscut, ambapo
watahakiki na kukabidhiwa Watanzania wote sitini na nne (64) na
wataruhusiwa kuingia nchini Oman na kuelekea Tanzania” alimaliza Mhe. Ali Ahmed
Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Mgogoro wa Yemen unaoendelea
baina ya maafisa wa polisi waaminifu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Ali
Abdullah Saleh, na makundi ya usalama yanayomuunga mkono rais wa sasa, Abed
Rabbo Mansour Hadi, umeua mamia ya watu na kujerui maelfu.
Mhe. Membe ametoa rai kwa
Watanzania wote wenye ndugu au jamaa nchini Yemen kuchukua tahadhari na
kuwataarifu watafute msaada kupitia Ubalozini Muscat ili kujihakikishia usalama
wao. Aidha ametoa tahadhari kwa Watanzania wanaotegemea kusafiri kwenda Yemen,
kusitisha safari zao hadi hali ya usalama itakaporejea.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es
Salaam
16 Aprili, 2015
0 comments:
Post a Comment