Tatizo sugu na la muda mrefu
la mbwamwitu kushambulia mifugo ya
wananchi katika eneo la loliondo
wilayani ngorongoro limepata ufumbuzi baada ya wadau wa uhifadhi wa ndani
na nje kukubali ombi la Mh.Rais Dr.
Jakaya Kikwete la kutoa fedha kwa ajili ya kuwakamata mbwamwitu wote walioko katika maeneo ya
wananchi na kuwarudisha hifadhini.
Wadau wa nje walioanza
kukubali kusaidia kazi hiyo ni pamoja shirika la Grumet Fund na wadau wa ndani ni pamoja na shirika la
hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mashirika ambayo kwa
kuanzia yameahidi kutoa jumla ya milioni
mia mbili.
Mratibu wa mradi huo wa kuwaondoa
wanyama hao kwenye makazi ya watu Dr. Ernest Mjingo na meneja wa mradi Bw.Emanuel Masenga
wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni gharama kubwa ya uendeshaji hasa vitendea
kazi vikwemo vifaa maalumu vya mawasiliano ya
kuratibu mwenendo wa wanyama hao.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya
utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) inayosimamia mradi huo Dr.Simino Mduma amesema
hadi sasa makundi matano yenye mbwamwitu zaidi 60 yamekamatwa na kurejeshwa hifadhini hatua ambayo licha ya
kuashiria uwepo wa wanyama hao walioko
kwenye hatari ya kutoweka ni faraja kubwa kwa sekta ya utalii.
Aliposhiriki zoezi la
kurejesha kundi la tano lenye mbwamwitu 13 waliokamatwa katika eneo la loliondo Rais wa Tanzania Mh. Dr
Jakaya Kikwete aliwaomba wadau wa uhifadhi wa
nje na ndani kusaidia zoezi hilo
kuwadhibiti wanyama hao ambao licha ya kuwasabaabishia wafugaji hasara ya kula mifugo yao wana faida
kubwa katika utalii.
0 comments:
Post a Comment