Kamati ya Bunge ya ardhi,maliasili na mazingira ya Tanzania
imeipongeza afrika kusini kwa kutumia rasilimali zake vizuri kujenga mundombinu
bora ya kuwezesha watalii kufika katika ncha ya kusini kabisa ya bara la afrika
iitwayo CAPE POINT licha ya barabara hizo kupita katika maeneo hatari ikiwemo
milima na majabali makubwa ya mawe katika mwambao wa bahari ya ATLANTIC.
Wakiongea baada ya kufika katika ncha hiyo ya kusini ya bara la
afrika ambapo pia bahari mbili hukutana yaani bahari ya hindi yenye maji ya
joto na bahari ya ATLANTIC yenye maji baridi,wajumbe wa kamati hiyo akiwemo
mwenyekiti wake JAMES LEMBELI na DK PETER KAFUMU wamesema licha ya kwamba
barabara hizo zinapita kwenye milima hiyo ya hatari lakini nchi hiyo kwa
kutumia rasilimali zake imezijenga kwa ustadi mkubwa na kuwezesha safari za
watalii kuwa za usalama.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ya bunge walioko kwenye ziara
hiyo ya mafunzo nchini afrika kusini wamesema uwekezaji mkubwa katika sekta
hiyo, umeiwezesha nchi ya afrika kusini kuwa ya pili kwa idadi kubwa ya watalii
barani afrika baada ya misri watalii ambao wanaliwezesha taifa hilo kupiga
hatua kubwa kwa maendeleo ikilinganishwa na tanzania ambayo imekuwa ikipata
watalii wachache kwani licha ya kuwa na maliasili nyingi lakini miundombinu
yake haijawa rafiki kwa watalii.
Kamati hiyo ya bunge pia imefika katika eneo la CAPE OF GOO HOPE ama
Rasi ya tumaini jema maeneo ambayo wavumbuzi wa kale akiwemo VASCO DAGAMA na BATHOLMEW
DIAZ walifika mwanzoni mwa miaka ya 1800 wakiwa katika harakati za kufika india
kwa njia ya bahari kutokea afrika ambao pia walijenga minara kuyatambulisha
kama maeneo muhimu kimataifa na nchi ya afrika kusini imeyafanya kuwa sehemu ya
hifadhi ya taifa ya milima meza au TABLE MOUNTAIN ambayo ni miongoni mwamaajabu
saba ya asili ya dunia.
0 comments:
Post a Comment