Image
Image

NEWS ALERT:Mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba afikishwa mahakama ya kisutu pamoja na wanachama 30 kwa kosa la kuratibu maandamano bila utaratibu maalum.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi  CUF  Profesa IBRAHIM HARUNA LIPUMBA na wanachama we ngine 30  wa chama hicho,  leo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam waki shtakiwa kwa kosa la kuandamana  bila kufuata utaratibu .
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar  ambaye  pia ni  Katibu Mkuu wa  - CUF -  maalim SEIF SHARIF HAMAD   ni miongoni mwa viongozi  wanaohudhiria kesi hiyo  inayomkabili mwenyekiti  wa chama hicho .
Profesa LIPUMBA na wafuasi 30 wa CUF wamefunguliwa mash i taka ya kula njama, kukukusanyika na kuandamana bila ya kibali na  kwa sasa wapo nje kwa  dhamana .
Katika tukio la maandamano hayo , viongozi na wafuasi wa CUF walipigwa na kukamatwa na polisi kwa madai ya kuandamana bila kibali wakati wakiadhimisha mauaji ya wenzao waliouawa na polisi mwaka 2001.
Wafuasi hao walikuwa wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar mwaka 2000.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment