Mwenyekiti wa tume
hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva ameyasema hayo jijini dar es salaam ambapo
amesema tume imepokea BVR 248 na kufanya jumla ya mashine hizo kufikia 498 na
kuongeza kuwa muda mfupi ujao watapokea nyingine 1600 zinazowasili kwa ndege ya
kukodi kutoka Dubai.
Aidha
jaji lubuva ametaja awamu ya pili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura itaendelea April 24 mwaka huu, siku ambayo pia watapokea BVR
nyingine 1600 ambazo amesema zitaharakisha kasi ya uandikishaji kwani wataweza
kuandikisha mikoa mingi kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa awamu ya pili ya
zoezi la BVR itakuwa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa.
Kwa
upande wake naibu katibu mkuu kitengo cha daftari la wapiga kura Sisti Karia
amesema endapo wangekuwa na mashine za bvr za kutosha wangezigawa kwenye
halmashauri nchi nzima hivyo wangeweza kuendesha zoezi la kuandikisha watu kwa
siku 28 tu nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment