Awali
akimkaribisha mgeni rasmi,mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu Prof . Penina Mlama
amesema katika tamasha hilo litaangalia mambo mbalimbalu kubwa ni kujua kiini
hasa cha migogoro ardhi na uwekezaji inayojitokeza kwa wingi hapa nchi na
afrika kwa ujumla.
Akizungumza
katika ufunguzi wa tamasha la siku tatu la kidoga cha mwalimu,Prof
Mukandara amesema idadi kubwa ya waafrika hawaelewi matokeo ya
mageuzi ya kiuchumi na ubinafsishaji katika kuboresha maisha yao licha ya
kuwepo kwa ukuaji wa haraka pato la taifa.
Aidha
katika tamasha hilo,waziri wa maliasili na utalii mhe. Lazaro Nyarandu amesaini
hati ya jengo la ukumbi wa Nkruma kuwa miongoni mwa tunu ya utamaduni ya taifa
kutokana na historia kubwa ya ukumbi huo katika kuenzi uhuru wa majadiliano.
0 comments:
Post a Comment