Agizo
hilo limetolewa na mkuu wa mkoa huo,Elaston Mbwilo Katika kijijiji cha lamadi
wakati alipokwenda kuwatembelea wananchi hao waliokumbwa na mafuriko hayo
ambapo amesema eneo hilo kwa hivi sasa halifai tena kwa makazi kwani wananchi
wakiachwa wakaendelea kuishi hapo kila mwaka watakuwa wanakumbwa na mafuriko
kutokana na mabadiriko ya tabia nchi.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa amewaomba wananchi hao kuendelea kuwa na subira kwani
serikali bado inaendelea kufanya tathimini ya mafuriko hayo na kwamba
ikikamilisha watalewa chakula ambapo pia amewaomba wasamalia wema,mashairika na
taasisi zilizoguswa na janga hilo kuendelea kutoa misaada kwa wananchi hao.
Wiki
iliyopita wananchi wa kijiji hicho walikumbwa na mafuriko ambapo nyumba 288
zilibomolewa,baadhi ya mifugo kama kondoo na kuku kusombwa na maji huku zaidi
ya kaya 1686 zikiwa hazina mahali pa kuishi.
0 comments:
Post a Comment