Ujenzi huo wa maabara ni
utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya
Mrisho Kikwete,ambaye ametaka kila kila
mkuu wa wilaya kusimamia ujenzi wa maabara tatu katika shule zote za sekondari.
Agizo hilo la serikali
wilayani bunda limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Bw.Joshua Mirumbe,baada ya kupokea mifuko mianne ya
saruji ambayo imetolewa na mmoja ya wakazi wa
bunda kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 81 vya maabara katika shule 27 za
sekondari wilayani Bunda.
Kwa upande wake Mkazi huyo wa
bunda ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Huduma ya jijini mwanza Bw Zully Nanji,akizungumza
baada ya kukabidhi sheena hiyo ya mifuko ya
saruji,amesema kuwa kama mzawa wa wilaya
ya bunda,ameguswa katika
kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa ajili ya kuharakisha maendelea ya jamii na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment